Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa zaidi ya watoto wanaishi nje ya nchi zao kama wakimbizi na wahamiaji:UNICEF Ripoti

Binti wa miaka 7 akiwa amembeba mdogo wake katika kambi ya wahamiaji wa ndani jimboni Kandahae, Kusinimagharibi mwa Afghanistan
© UNICEF Afghanistan
Binti wa miaka 7 akiwa amembeba mdogo wake katika kambi ya wahamiaji wa ndani jimboni Kandahae, Kusinimagharibi mwa Afghanistan

Idadi kubwa zaidi ya watoto wanaishi nje ya nchi zao kama wakimbizi na wahamiaji:UNICEF Ripoti

Amani na Usalama
  • Waasichana wanahama zaidi kuliko wavulana
  • Watoto wote wa kiume na kike wapo hatarini kufanyiwa vitendo kinyume na haki za binadamu
  • Kuna ongezeko mara 10 la watoto kuvuka mipaka
  • Afghanistan inashika namba 1 kati ya nchi 10 zenye watoto wanaohama nchi zao

Ripoti mpya ya matokeo ya utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo inaonyesha kwamba jinsia yam toto muhamiaji au mkimbizi kutokana na mizozo na vita ni muhimu sana haswa kwa jinsi atakavyochukuliwa katika nchi itakayomuhifadhi.

Ripoti imesema karibu nusu ya Watoto ambao wanaishi nje ya nchi zao walikozaliwa ni wasichana na wako katika hatari ya kunyanyaswa, kutumbukia katika biashara haramu ya binadamu na ukatili wa kingono, huku wavulana wakiwa katika hatari ya kuingizwa jeshini katika vita na kusafiri bila mzazi au mlezi.

 Jinsia yako ndio faida na hatari yako
 

Ripoti hiyo imejikita zaidi katika kuangalia hatari, mahitaji na fursa zinavyoweza kuunda maisha ya wasicha na wavulana wakimbizi na wahamiaji.

Na inasema hivi sasa wasichana na wavulana wengi zaidi wanakimbia makwao kwa sababu mbalimbali ikiwemo miozo na vita.
Mwaka jana UNICEF inasema watoto milioni 35.5 wa umri wa chini ya miaka 18 walikuwa wakiishi nje ya nchi zao za kuzaliwa na wasichana na wavulana wengine milioni 23.3 walitawanywa ndani ya nchi zao.

Pia ripoti imeongeza kuwa watu takriban milioni 15 wapya wametawanywa katika kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni sawa na watu wapya 41,000 wanaotawanywa kila siku.
Na hii inamaanisha kwamba leo hii karibu wasichana na wavulana milioni 60 wamevuka mipaka kuhamia nchi nyingine au kulazimika kutawanywa ndani ya nchi zao .
Kwa mujibu wa ripoti idadi hiyo ni karibu mara 10 ikilinganishwa na mwaka 2015 wakati UNICEP ilipochapisha ripoti kuhusu watoto waliotawanywa.

Baba akiwa na binti yake katika kambi ya wakimbizi wa ndani, watu milioni 18 nchini Afghanistan wanahitaji msaadawa kibinadamu
© UNICEF Afghanistan
Baba akiwa na binti yake katika kambi ya wakimbizi wa ndani, watu milioni 18 nchini Afghanistan wanahitaji msaadawa kibinadamu

 Njia nyingine na uzoefu wa uhamiaji hunategemea jinsia.  

Mathalani ripoti inasema mwaka 2020, watoto 9 kati ya 10 wasioambatana na wazazi au walezi waliosaka hifadhi Ulaya walikuwa wavulana na 2 kati ya 3 walitoka Afghanistan.
Afghanistan inashikilia namba 1 kwenye orodha ya nchi 10 zenye idadi kubwa zaidi ya watoto wasioambatana na wazazi au walezi wanaotafuta hifadhi Ulaya. Wavulana wengi wa Afghanistan wamevuka mipaka ya nchi yao kuliko wasichana.

Ulimwenguni kote wasichana na wavulana wanaweza kuhama au kuzikimbia nchi zao  kwa sababu tofauti mfano wavulana mara nyingi wanatarajiwa kuchukua jukumu la kusaka mkate, wakati wasichana wanaweza kuhama au kukimbia makwao kama mbinu ya kuchelewesha ndoa za mapema au unyanyasaji wa kingono.

Miongoni mwa waathiriwa wanao gundulika kwa usafirishaji haramu wa binadamu, wasichana ni wengi kuliko wavulana kwani ni idadi ya 4 na  3. Wasichana wana uwezekano mkubwa wa kusafirishwa kwa ajili ya masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, wakati wavulana wengi ni kwa ajili ya kufanyishwa kazi za shuruti.