Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wabaini makadirio ya wakimbizi wa ndani Tigray na maeneo jirani

IOM inasema kuna zaidi ya wakimbizi wa ndani 131,000 kwenye mikoa ya Tigray, Amhara na Afar nchini Ethiopia
IOM Ethiopia
IOM inasema kuna zaidi ya wakimbizi wa ndani 131,000 kwenye mikoa ya Tigray, Amhara na Afar nchini Ethiopia

Utafiti wabaini makadirio ya wakimbizi wa ndani Tigray na maeneo jirani

Wahamiaji na Wakimbizi

Zaidi ya watu 131,000 wametawanyika katika maeneo 39 yanayofikika katika mikoa ya Tigray, Afar na Amhara nchini Ethiopia.

 

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM, ikisema ni takwimu rasmi za mwanzo kabisa tangu eneo la kaskazini mwa Ethiopia lianze kukumbwa na mapigaon mwezi Novemba mwaka jana wa 2020.
Hata hivyo shirika hilo linasema takwimu hizo si kiashiria cha idadi ya watu wakimbizi wa ndani kutokana na janga la mapigano, bali zinawakilisha idadi ya wakimbizi wa ndani waliomo kwenye maeneo yaliyofikiwa na utafiti huo.

Takribani asilimia 70 wa Tigray, asilimia 26 Afar na asilimia 5 wako mkoa wa Amhara.

Tweet URL

“Idadi kubwa ya watu hao ni wanawake na watoto na wanaripotiwa kuhitaji malazi, chakula na huduma za maji safi na salama ya kuywa,” imesema taarifa ya IOM iliyotolewa leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Tangu kuanza kwa mapigano, IOM imekuwa ikifuatilia hali ya kibinadamu na ukimbizi wa ndani kupitia tathmini yake ya kimaeneo ambayo inachukua idadi ya wakimbizi wa ndani, maeneo waliko na mahitaji yao, ambapo utafiti wa sasa ulifanyika kati ya tarehe 22 Desemba mwaka jana na taree 14 mwezi Januari mwaka huu.

Utafiti huo ulibaini kaya 30, 383 zilizokimbia makazi yao ambapo IOM imesema itapanua wigo wa utafiti ujao ili ufikie maeneo zaidi ya ndani ya Kaskazini mwa Ethiopia, kazi ambayo itafanywa kwa ushirikiano na kamisheni ya usimamizi na uratibu wa majanga nchini Ethiopia.