Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni 1 wametawanywa katika maeneo 178 kwenye jimbo la Tigray

Eneo la Tigray linakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleao nchini Ethiopia
© UNICEF/Zerihun Sewunet
Eneo la Tigray linakabiliwa na changamoto nyingi za kimaendeleao nchini Ethiopia

Zaidi ya watu milioni 1 wametawanywa katika maeneo 178 kwenye jimbo la Tigray

Wahamiaji na Wakimbizi

Zaidi ya watu milioni 1 wametawanywa katika maeneo 178 kwenye jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia na majimbo ya jirani ya Afar na Amhara kwa mujibu kwa takwimu zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji IOM.

Takwimu hizi zimekuwa zikikusanywa kila mwezi tangu mzozo ulipozuka Novemba 2020 na kitengo cha IOM cha tathimini ya dharura ya watu kutawanywa, ESA. 

Tathmini iliyoendeshwa kuanzia tarehe 2 Machi hadi tarehe 23 Machi imeonesha kwamba kuna wakimbizi wa ndani milioni 1.05 jimboni Tigray pekee,  wengine 45,343 jimboni Afar na 18,781 jimboni Amhara. 

IOM inasema takwimu hizi zinadhihirisha kwamba wakimbizi wa ndani wanakimbilia kwenye miji mingine kwenda kusaka msaada wa kibinadamu na huduma zingine za muhimu na hii ni tathimini ya 4 kufanywa na IOM katika eneo hilo. 

Sasa IOM imetoa ombi la dola milioni 58 kwa ajili ya kusaidia kwenye mgogoro wa Ethiopia lakini dola milioni 22 kati ya hizo zitatumika kusaidia mahitaji ya wakimbizi wa ndani nchini Msumbiji.