Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yazindua mkakati wa kushughulikia athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19

Janga la corona limekuwa na athari katika uchumi kote ulimwenguni.
UNDP Eurasia/Karen Cirillo
Janga la corona limekuwa na athari katika uchumi kote ulimwenguni.

UN yazindua mkakati wa kushughulikia athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19

Afya

Umoja wa Mataifa leo umezindua mkakati wa kushughulikia uwezekano wa athari kubwa za kijamii na kiuchumi zitakazosababishwa na janga la kimataifa la mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 na kuanzisha mfuko wa kuzisaidia nchi za kipato cha chini na cha wastani.

Ugonjwa huo ulioanzia China mwezi Desemba mwaka jana umewaathiri zaidi ya watu 693, 224, kote duniani.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO virusi hivyo sasa vimesambaa katika nchi  na maeneo 203 duniani na idadi kubwa ya wagonjwa imerekodiwa Marekani, Italia, China na Hispania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterrees amesema “virusi hivyo vipya vya  Corona, COVID-19 vinashambulia jamii, kuua wat una kusambaratisha Maisha. Pia vinauwezekano wa athari za muda mrefukwa uchumi wa dunia na uchumi wa kila nchi sasa unayumba.”

Katika ripoti mpya iliyopewa jina “Kushirikiana wajibu, mshikamano wa kimataifa:kukabiliana na athari za kijamii na kiuchuni za COVID-19” Katibu Mkuu ametoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za pamoja kushughulikia athari na kupunguza madhila ya janga hili kwa watu.

Ripoti imeelezea kasi na kiwango cha mlipuko huo, ukubwa wa idadi ya wagonjwa na athari za kijamii na kiuchumi zilizosababishwa na COVID-19 ugonjwa ambao hadi sasa umeua watu 33,106. Guterres amesema “COVID-19 ni jaribu kubwa kabisa kuwahi kutukabili sote tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, huu ni mgogoro wa kibinadamu unahitaji hatua za pamoja, maamuzi ya pamoja, jumuishi na sera bunifu kutoka kwa nchi zilizoendelea kiuchumi duniani na msaada mkubwa wa kifedha na kiufundi kwa nchi masikini kabisa na kwa nchi na watu wasiojiweza.”

Hatua za kuchukua

Ripoti hii imetoka baada ya shirika la fedha duniani IMF kutangaza kwamba dunia imetumbukia katika mdororo wa uchumi ambao ni mbaya kama ulivyokuwa wa 2009 au zaidi. Ripoti inatoa wito wa hatua za pamoja za kimataifa ambazo ni saw ana asilimia 10 ya pato la kimataifa.

Mfumo wa Umoja wa Mataifa na mtandao wake mzima wa kimataifa, kikanda na katika ofisi zake za nchi mbalimbali zinazohusika na masuala ya amani, haki za binadamu, maendeleo endelevu na hatua za kibinadamu zitazisaidia serikali zote na washirika katika hatua za kupambana na janga hili na zile za kujikwamua.

Mfuko maalum waanzishwa

Na kwa mantiki hiyo Katibu mkuu ameanzisha mfuko maalum kwa ajili ya hatua za kupambana na COVID-19 na kujikwamua katika janga hilo “COVID-19 Response and Recovery Fund”. Mfuko huo utasaidia juhudi za nchi za kipato cha chini na cha wastani. Mtazamo wake unazingatia Umoja wa Msataifa ulivyobadilishwa kwa kuwa na uratibu wa mashirika na sekta mbalimbali kwa kipaumbele cha kitaifa na hatua za mashinani kushughulikia kushughulikia athari za kijamii na kiuchumi za mgogoro wa COVID-19.

Mfuko huo utategemea zaidi uongozi wa waratibu na timu za Umoja wa Mataifa katika nchi mbalimbali kuzisaidia na kuziwezesha serikali katika mgogoro hu una wakati wa kujikwamua na athari zake.