Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji na mauaji ya kimbari dhidi ya Rohingya vinaendelea Myanmar:Darusman

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kusaka ukweli wa ukiukwaji wa haki za binadamu Myanmar
Picha na Umoja wa Mataifa /Paulo Filgueiras
Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kusaka ukweli wa ukiukwaji wa haki za binadamu Myanmar

Ukiukwaji na mauaji ya kimbari dhidi ya Rohingya vinaendelea Myanmar:Darusman

Haki za binadamu

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Mataifa ya kutafuta ukweli wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Myanmar, Marzuki Darusman amesisitiza kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya kimbari vinaendelea dhidi ya jamii ya watu wa kabila la Rohinya.

Akizungumza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo kuwakilisha kile walichobaini nchini Myanmar kuhusu ukiukwaji wa haki dhidi ya kalbila la Rohingya Bwana Darusman amesema maovu yanaendelea kufanyika dhidi ya watu wa kabila la Rohingya nchini humo hata hivi sasa  na kwamba

(SAUTI YA MARZUKI DARUSMA ) 

"Msimamo mgumu wa serikali ya Myanmar kwa kiasi kikubwa ndio kikwazo , kuendelea kwake kutokubali hali halisi na kujitetea kwa mwamvuli wa uhuru wa kitaifa na pia kupinga maelezo ya kurasa 444 yaliyojaa ukweli na mazingira ya ukiukwaji wa haki za binadamu hivi karibuni , huo ni uhalifu mkubwa sana chini ya sheria za kimataifa.”

ameonya kuwa kinachoendelea hivi sasa kwa hakika ni mauaji ya kimbari dhidi ya Rohinya

(DSAUTI YA MARZUKI DARUSMAN  )

”Ninasisitiza kwamba maovu yanaendelea kutendeka leo na hata wakati huu, jamii ya Rohinya iliyosalia inaendelea kutaabika kwa kiasi kikubwa kwa vikwazo vikali, mateso, ukandamizaji na hakuna mabadiliko yoyote kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita tangu Agosti 2017. Ni mauaji ya kimbari ndiyo yanayoendelea kwa wakati huu.”

Rohingya wavuka mto Naf ili kufikia kambi za wakimbizi nchini Bangladesh
© UNHCR / Andrew McConnell
Rohingya wavuka mto Naf ili kufikia kambi za wakimbizi nchini Bangladesh

Ameongeza kuwa mahitaji manne kati ya matano ya  kutokea kwa mauaji ya kimbari yametekelezwa nchini Myanmar ikiwemo mauaji, ukatili , mazingira ya uchochezi ya kutaka kulitokomeza kundi fulani na pia kuanzisha hatua za kuzuia kizazi fulani.

Pamoja na yote hayo amesema ukweli unasalia palepale, dhamisha ya mauaji ya kimbari ambayo amesema tume hiyo imeibaini na sasa imedhamiria kuwafikisha mjenerali sita wa jeshi la Myanmar waliobainiwa na tume mbele ya mahakalama ya kimataifa ya uhalifu ICC, au kwenye mahaka nyingine ili washitakiwe wakianza na kamanda mkuu Min Aung Hlaing.

Na mapema leo mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar Yanghee Lee akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani amesema serikali ya Myanmar imeendelea kuwa kaidi

(SAUTI YA YANGHEE  LEE)

“Serikali imeendelea kuonyesha kutojali na kutokuwa na uwezo wa kuanzisha demokrasia kamili ambayo watu wake wote wataweza kufurahia haki na uhuru wao. Haitimizi haki na utawala wa sheria . Utawala wa sheria ambao mara kadhaa imerejea kusema watu wote nchini Myanmar wanauzingatia. Hata hivyo hiyo sio hali halisi , endapo utawala wa sheria ungezingatiwa watu wote nchini Myanmar bila kujali hadhi zao wangewajibishwa sawia na mkono wa sheria, kusingekuwepo na ukwepaji sheria na sheria isingetumika kama silaha ya ukandamizaji.”

Mwezi Machi mwaka jana Baraza Kuu la Hak iza binadamu la Umoja wa Mataifa lilianzisha tume maalumu ili kupata ukweli nchini Myanmar na mazingira yanayodaiwa kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili unaotekelezwa na jeshi na vikosi vingine vya usalama.