Ukatili Myanmar waendelea kuathiri warohingya

4 Januari 2018

Ukatili na uvunjifu wa  haki za binadamu nchini Myanmar vinaendelea kuathiri maisha ya watu wa kabila la Rohingya. Taarifa zaidi na Patrick Newman.

(Taarifa ya Patrick Newman)

Mwenyekiti wa tume huru ya kimataifa ya kusaka taarifa nchini Myanmar, FFMM Marzuki Darusman amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi baada ya timu yake kukutana na warohingya huko Cox Bazar nchini Bangladesh ambako wamesaka hifadhi.

(Sauti Marzuki Darusman)

‘‘Hali haijatengemaa Myanmar kikamilifu. Tunaendelea kusikia uchomaji moto ukiendelea, na makataa pia. Hili linaendelea kuathiri jamii hii.’’

Amesema ukatili huo pia unajumuisha mauaji ya halaiki, ubakaji wa makundi na watu kukamatwa kiholela na hivyo..

(Sauti Marzuki Darusman)

‘’Ushahidi kwa hakika utatumiwa kuandaa hitimisho na mapendekezo kwenye Baraza la Haki za Binadamu, yatajumuisha hatua za kinidhamu kwa wahusika wakuu wa ukatili huu wa halaiki.”

Mwezi Disemba mwaka jana, wajumbe watatu wa tume ya FFMM, walizuru Malaysia kwa siku tano ambapo walikutana na jamii za wakimbizi. Ripoti yao itawasilishwa mbele ya Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwaka huu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter