Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel lazima ichunguze mauaji ya mwanamke wa kipalestina Ukingo wa magharibi:Mladinov

Halamish, makazi ya Israel, katika eneo a Kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, karibu na kijiji cha wa Palestina cha Nabih Saleh.
Photo: UNICEF/Mouhssine Ennaimi
Halamish, makazi ya Israel, katika eneo a Kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, karibu na kijiji cha wa Palestina cha Nabih Saleh.

Israel lazima ichunguze mauaji ya mwanamke wa kipalestina Ukingo wa magharibi:Mladinov

Amani na Usalama

Mamlaka ya Israel imetolewa wito wa kuwawajibisha kisheria wale waliohusika na shambulio ambalo llimekatili maisha ya mwanamke mmoja wa Kipalestina na kumjeruhi mumewe katika Ukingo wa magharibi.

Wito huo umetolewa leo jumapili mjini Jerusalemkupitia taarifa  ya mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov, wakati akilaani vikali  shambulio dhidi ya Aisha Al-Rabi, alieuawa Ijumaa kwa mawe ambayo yanadaiwa kurushwa na washambuliaji wa Israel. Mwanamke huyo ameacha watoto wanane.

 Afisa huyo amesema anatambua kwamba uchuguzi umeshaanza na ameitaka serikali ya Israel kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya haki na kuwajibishwa. Ameongeza kuwamashambulio kama hayo hayana tija yoyote nayanaweza tu kulitumbukiza eneo hilo katika duru nyingine ya ghasia ambazo zitahujumu hatua za kuleta amani kati ya wa Palestina na Israeli.

Pia amemutolea wito kwa pande zote kulaani vitendo vya ghasia na kupinga ugaidi.

Hadi sasa hakuna tarifa zozote zilizotolewa kuhusu kilichipelekea mauaji hayo .