Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upanuzi wa makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi unakiuka sheria:Mladevov

Nickolay Mladenov, Mratibu Maalum wa mchakato wa amani Mashariki ya Kati  akihutubia Baraza la Usalama la UN
UN /Loey Felipe
Nickolay Mladenov, Mratibu Maalum wa mchakato wa amani Mashariki ya Kati akihutubia Baraza la Usalama la UN

Upanuzi wa makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi unakiuka sheria:Mladevov

Amani na Usalama

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Nickolay Mladenov amesema kitendo cha Israel kuendelea kupanua wigo wa makazi ya walowezi katika eneo linalokaliwa la Palestina kwenye Ukingo wa Magharibi ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo jumatano Mladenov amesema “Mamlaka ya Israel imeidhinisha katika siku mbili zilizopita ujenzi wa makazi 2, 400 katika eneo la Area C kwenye Ukingo wa Magharibi”

Ameongeza kuwa upanuzi huo wa makazi ya walowezi hauna haki yoyote ya kisheria n ani ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Na kusisitiza kwamba kuendelea na ujenzi huo Ukingo wa Magharibi kunaathiri fursa za kuundwa kwa taifa la Palestina kwa misingi ya maazimio ya Umoja wa Mataifa , kama sehemu ya majadiliano ya suluhu ya kuwa na mataifa mawili.

Kwa mantiki hiyo Bwana Mladenov amesema ujenzi huo usitishwe kabisa mara moja.