Ukingo wa Magharibi

Mchakato umekwama Mashariki ya Kati, ghasia zashamiri, amani mashakani- Mladenov

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mchakato wa amani Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov ameonya kuwa hatua za haraka zinahitajika ili kurejesha mchakato wa amani kwenye eneo hilo kwa mujibu wa maazimio ya Umoja wa Mataifa huku akitoa wito kwa viongozi wa pande zote za Israel na Palestina kuchukulia hatua makundi yenye misimamo mikali.

Upanuzi wa makazi ya walowezi Ukingo wa Magharibi unakiuka sheria:Mladevov

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Nickolay Mladenov amesema kitendo cha Israel kuendelea kupanua wigo wa makazi ya walowezi katika eneo linalokaliwa la Palestina kwenye Ukingo wa Magharibi ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Waisraeli waliowashambulia wapalestina wawajibishwe-OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imesikitishwa na vurugu za mashambulizi ya muda mrefu dhidi ya wapalestina ikirejelea shambulizi la hivi karibuni katika kijiji cha Al Mughayyir kilichoko katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Huku misaada ikipungua, mwaka wa 2018 umeshudia ongezeko la majeruhi kwa wapelestina: OCHA

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada OCHA, kwa mwaka huu wa 2018, vikosi vya Israel vimewauwa wapalestina 295 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 29,000, hii ikiwa ndiyo idadi kubwa ya vifo kuwahi kutokea kwa mwaka mmoja tangu mgogoro wa Gaza uanze mwaka 2014 na pia kuwa na idadi kubwa ya majeruhi tangu tangu OCHA ianze fuatilia majeruhi katika eneo la Palestina linalokaliwa, maarufu kama oPt.

Ukata kulazimu WFP kukata msaada kwa baadhi ya wapalestina mwakani: WFP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linasaka  dola milioni 57  ili liweze kuendelea  kutoa msaada mwaka ujao kwa  wapalestina 360,000 wanaoishi ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Palestina inahitaji dola milioni 350 kushughulikia misaada ya kibinadamu: OCHA

Mpango mkakati wa msaada wa kibinadamu HRP wa mwaka 2019 umetoa ombi la dola milioni 350  ili kutoa huduma za msingi kama chakula, ulinzi, huduma za afya, malazi, maji na usafi kwa Wapalestina milioni 1.4 ambao wamebainika kuwa na mahitaji makubwa ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Maghariki likiwemo eneo la Jerusalem Mashariki.

Israel lazima ichunguze mauaji ya mwanamke wa kipalestina Ukingo wa magharibi:Mladinov

Mamlaka ya Israel imetolewa wito wa kuwawajibisha kisheria wale waliohusika na shambulio ambalo llimekatili maisha ya mwanamke mmoja wa Kipalestina na kumjeruhi mumewe katika Ukingo wa magharibi.