Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni historia, mkakati wa kwanza kabisa wa kimataifa wa uhamiaji tumeukalimisha: Lajčák

Miroslav Lajčák, Rasi wa kikao cha 72 cha baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (kushoto) akiwa amesimama na Balozi Juan José Gómez Camacho wa Mexico( Katikati) na Jürg Lauber wa Uswis ( Kulia) muwezeshaji mwenza wa majadiliano kuhusu mkakati wa kimataifa wa uhe
Picha na UN/ Mark Garten
Miroslav Lajčák, Rasi wa kikao cha 72 cha baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (kushoto) akiwa amesimama na Balozi Juan José Gómez Camacho wa Mexico( Katikati) na Jürg Lauber wa Uswis ( Kulia) muwezeshaji mwenza wa majadiliano kuhusu mkakati wa kimataifa wa uhe

Ni historia, mkakati wa kwanza kabisa wa kimataifa wa uhamiaji tumeukalimisha: Lajčák

Wahamiaji na Wakimbizi

Mkakati wa kimataifa kuhusu uhamiaji salama  na wa mpangilio umekamilishwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani .

Hii ni mara ya kwanza kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kushikamana kwa pamoja ili kujadili makubaliano yatakayozingatia nyanja zote za uhamiaji wa kimataifa kikamilifu na kwa kina.

Mkakati huo wa kimataifa ni mjumuiko wa majadiliano na mashauriano kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na watendaji kama vile viongozi wa ngazi za kijamii, wawakilishi wa asasi za kiraia na wahamiaji wenyewe; wakiorodhesha na kutafakari maoni yaliyowasilishwa na pia mazungumzo ya kiserikali.

Hali ilivyo katika maeneo ya kushikilia wahamiaji na wasaka hifadhi. Hapa ni Libya nje kidogo ya mji mkuu, Tripotli.
UNICEF/Alessio Romenzi
Hali ilivyo katika maeneo ya kushikilia wahamiaji na wasaka hifadhi. Hapa ni Libya nje kidogo ya mji mkuu, Tripotli.

Kwa jumla, mchakato huu wa wazi na jumuishi uliofanyika kwa zaidi ya miezi 18 umefanya kuwepo kwa majadiliano na kujifunza kusiko kwa kawaida kwa washiriki wote  kuhusu  hali halisi ya uhamiaji wa kimataifa.

Muafaka huu sasa  unaunda msingi wa kuboresha utawala na uelewa wa uhamiaji wa kimataifa, kukabiliana na changamoto za sasa zinazohusiana na uhamiaji, na kuimarisha mchango wa wahamiaji na uhamiaji kwenye maendeleo endelevu.

Akiita siku ya leo kuwa ni ‘Wakati wa kihistoria’ Rais wa kikao cha 72 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa Miroslav Lajčák, amesema uwezo wa mkakati huu wa kimataifa ni mkubwa akiongeza kuwa “Utaweza kutuongoza kutoa katika hali ya kukabili na kuingia katika hali inayofa’’

Pia amesema utaweza kusaidia kudhihirisha faida za uhamiaji, kudhibiti hatari, kutoa jukwaa jipya kwa ajili ya ushirikiano, na pia unaweza kuwa chanzo muhimu cha kupata uwiano muafaka baina ya haki za watu na uhuru wa nchi. Mnano Desemba Lajčák amesema, utakuwa mfumo rasmi wa kwanza wa uhamiaji ulimwengu kuwahi kuushuhudia.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed (Maktaba)
UN Photo/Manuel Elías
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J Mohammed (Maktaba)

Akiongeza sauti yake  sauti yake kuhusu mkakati huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed, amesema “Uhamiaji unaibua masuala mengi muhimu, kuhusu uhuru wa nchi na haki za binadamu, uhusiano baina ya maendeleo na uhamiaji ma jinsi gani yakuunga mkono ushirikiano wa kijamii. Mkakati huu unaonyesha uwezekano wa utawala wa kimataifa, uwezo wetu wa kuja pamoja katika masuala yanayohitaji mshikamano wa kimataifa licha ya utata na changamoto zake.”

Naye Louise Arbour, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili ya uhamiaji wa kimataifa akaongeza “Uhamaji wa watu utakuwa nasi kama ilivyokuwa siku zote. Na mitazamo yake yenye tafran na ya hatari haiwezi kuruhusiwa kuwa ada. Utekelezaji wa mkakati huu utaleta usalama, utulivu na maendeleo ya kiuchumi yatakayomfaidisha kila mtu.’’

Makubaliano hayo yatapitishwa rasmi na nchi wanachama , kwenye mkutano wa kuidhinisha mfumo wa uhamiaji wa kimataifa utakaofanyika Marrakesh, Morocco, tarehe 10  na 11 Desember 2018.  Na Bi. Arbour  atakuwa Katibu Mkuu