Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji si karaha una faida zake: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na wandishi habari katika makao makuu ya UN 12 July 2018
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na wandishi habari katika makao makuu ya UN 12 July 2018

Uhamiaji si karaha una faida zake: Guterres

Wahamiaji na Wakimbizi

Uhamiaji si kero wala karaha bali ni suala jema la kimataifa kwani mamilioni ya wahamiaji ndio wanaosukuma gurudumu la  maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterresalipozungumza na waandishi habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Guterres ameyasemahayo wakati baraza kuu la Umoja wa Mataifa likijiandaa kukamilisha mchakato wa mkakati wa kimataifa kuhusu uhmiaji salama na wa mpango hapokesho Ijumaa na ukitarajia kuidhinishwa ramsi Desemba mwaka huu huko Marrakesh Morocco. Guterres amesisitiza kuwa

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

 “ Wahamiaji ni injini muhimu kwa maendeleo Idadi yao ni zaidi ya milioni 250 duniani kote ,na ni asilimia tatu ya idadi yote ya watu dunianiwakichangia jumla ya asilimia 10 ya pato la ndani duniani. Hata hivyo watu takriban 60,000  wamepoteza maisha baharini, ardhini na jangwani tangu mwaka wa 2000.Na kawaida wahamiaji na wakimbizi   hunyanyaswa na wakati mwingine kushambuliwa.”

Katibu Mkuu wa UN amesema mkakati huo mpya kuhusu wahamiaji una malengomakuu matatu.

 (SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

“Kwanza ni kuzielekeza será za maendeleo za kitaifa pamoja na ushirikiano wa kimataifa kutilia maanani wahamiaji na pia kutoa fursa kwa watu hao kufanya kazi na kuishi maisha ya kiutu nyumbani kwao.

Pili, ni muhimu kuimarisha ushirikiano wa kimataifa dhidi ya wasafirishajiharamu na wa kinyemela wa binadamu na kuwalinda waathirika. Usafirishaji haramu na wakinyemela wa watu ni kosa lakini si uhamiaji.

Tatu natoa wito kwa serikali kote duniani kuweka sheria zaidi zinazohusu uhamiaji.”

 

Mkakati huo kuhusu wahamiji na wakimbizi  ilipendekezwa mwaka 2016 ambapo mataifa 193 yaliidhinisha  tamko la New York ambalo ni linajikita katika jinsi ya kukabiliana na wimbi kubwa la  wahamiaji na wakimbizi duniani.

Mbali na suala hilo, Katibu Mkuu, pia amezungumzia unanyasaji na ukatili wa kingono ndani ya Umoja wa Mataifa akisema ameunda  kikosi maalum katika  idara inayohusika na masuala ya ndani ya Umoja wa Mataifa -OIOS- ili kujikita na uchunguzi dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa kingono na tayari nafasi sita za wachunguzi wa suala hilo zimeshaidhinishwa.

Baadhi ya hatua zilizochukuliwa, hadi sasa  amesema, ni kurahishisha  na kuharakisha mchakato wa kupokea ,na kushughulikia malalamiko ya unyanyasaji na ukatili wa kingono.