Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tunachagiza mabadiliko ya kisera ili kulinda bahari - Nancy Iraba

Nancy Iraba, mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam nchini Tanzania akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Lisbon Ureno kando ya mkutano wa kimataifa kuhusu Bahari.
UN Video

Tabianchi na mazingira

Mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu bahari unaendelea huko Lisbon, Ureno. Mkutano huu umeanza tarehe 27 mwezi huu wa Juni na utamalizika tarehe 1 Julai 2022. Kabla ya kuanza kwa kikao cha ngazi ya juu, mkutano ulitanguliwa na jukwaa la vijana likileta pamoja wanaharakati na wachechemuzi vijana kuhusu masuala ya baharí wakionesha ubunifu wao wa jinsi ya kutatua dharura ya baharí, kama alivyooiita Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres .Miongoni mwa washiriki ni kijana Nancy Iraba mwanasayansi wa masuala ya bahari kutoka Chuo Kikuu cha Dare es salaam nchini Tanzania. Hapa akihoijwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa anaelezea jukwaa linajikita na nini.