Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nidhamu ni sababu kuu ya mafanikio- Kiba

Mimi ingawa sikusoma lakini nidhamu imenisaidia kufika hapa nilipo.

Ali Kiba, mwanamuziki mashuhuri kutoka Tanzania. Pcha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Nidhamu ni sababu kuu ya mafanikio- Kiba

Utamaduni na Elimu

Vijana! Umoja wa Mataifa unasema kuwa kundi hili ndilo linalopaswa kuwa mstari wa mbele kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Hii ni kwa kuzingatia siyo tu wingi wao hivi sasa bali pia uwezo wao wa kubuni na kugundua teknolojia bora na fanisi za kufanikisha malengo hayo.

 Lakini je nini kinatakiwa zaidi tu ya kuwa kijana? Joseph Msami alizungumza na mwanamuziki mashuhuri kutoka Tanzania ambaye amevuma kitaifa na kimataifa. Mwanamuziki huyo si mwingine bali Ali Kiba ambaye hivi karibuni alitembelea Umoja wa Mataifa na hapa anaanza kwa kuelezea nini vijana wanapaswa kuzingatia ili wafanikiwe.