UN: Idadi ya raia waliouawa Ukraine yavuka 10,000
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kufuatilia Haki za Kibinadamu nchini Ukraine (HRMMU) umesema tangu kuanza kwa vita kati ya Urusi dhidi ya Ukraine tarehe 24 Februari 2022 zaidi ya raia 10,000 wamepoteza maisha nchini Ukraine kati yao watoto wakiwa ni 560 na zaidi ya 18,500 wamejeruhiwa.