Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 AGOSTI 2024

06 AGOSTI 2024

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha  anakuletea 

-Baada ya wiki kadhaa za maandamano makubwa na machafuko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya vijana na raia 300 #Bangladesh sasa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Gwyn Lewis, amesema kufikia leo utulivu kiasi umerejea nchini Bangladesh 

-Nchini Uingereza ambako maandamano yaliyochochewa na taarifa potofu na za uongo yanazidi kusambaa Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amesema ghasia hizo ikiwemo dhidi ya wasaka hifadhi zinashtusha na kila mtu bila utofauti wowote ana haki ya kujihisi salama kwenye jamii zao na kuishi huru bila hofu

-Leo ikiwa ni miaka 79 tangu MArekani iangushe bomu la atomiki la nyuklia huko Hiroshima nchini Japani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni ajabu kuwa silaha hizo na tishio lake la kuzitumia bado havijaondolewa kwenye matumizi. 

-Mada kwa kina leo inamulika juhudi za Tanzania katika kutumia sayansi na teknolojia kusongesha lengo namba 16 la maendeleo endelevu linalohusu masuala ya sheria na haki.

-Na mashinani tunabisha hodi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR katikashule ya Bombouthi ambayo inalishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa juhudi za kurejesha elimu

Audio Duration
10'27"