Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 MACHI 2024

18 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa unalowakumba waPalestina katika ukanda wa Gaza, na kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi ya Sudan Kusini. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? 

  1. Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya  hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani.
  2. Timu kutoka Kurugenzi ya Haki na Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo. 
  3. Assumpta Massoi wa Idhaa hii akizungumza na Khadija Mrisho, Afisa kutoka shirika la kiraia la kutetea haki ardhi kwa mwanamke LANDESA tawi la Tanzania yeye akiwa kiongozi wa kampeni ya kimataifa ya Linda Ardhi ya Mwanamke. Akiwa hapa New York, Marekani akishiriki mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, anaelezea kile walichojifunza. Lakini anaanza na kile kilichowaleta.
  4. Katika mashinani tutaelekea Ngong nchini Kenya kusikia ujumbe unaotia moyo wasichana waathirika wa mimba za utotoni.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'32"