Kenya: Mradi wa Teen Seed Africa warejesha matumaini ya elimu kwa wasichana waliopata mimba za utotoni
Umoja wa mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya ulizindua mwaka 2015 mradi wa kuwarejesha watoto shule walioacha kwa sababu moja au nyengine.
Kupitia mashirika mbalimbali kama Educate A Child, Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la idadi ya watu duniani UNFPA ilizindua miradi ya pamoja ya kuwarejesha watoto shule.
Utafiti wa hivi karibuni wa mashirika hayo umebainisha kuwa moja ya chanzo kikuu cha watoto wa kike kuacha shule ni mimba za utotoni na hususan watoto ambao wanaishi katika mitaa ya mabanda.