Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 JUNI 2023

29 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tukiwa tunaelekea maadhimisho ya pili ya siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili duniani leo tunaelekea nchini Uganda kuangazia hatua zinazopigwa kufuta kabisa usemi wa mitaani kuwa Kiswahili kilizaliwa Tanzania, kikafa Kenya na kisha kuzikwa Uganda. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za WHO, UNICEF na FAO. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma akitujuza walivyojiandaa kuadhimisha siku ya lugha ya Kiswahili duniani ambayo kilele chake ni Julai 7.

  1. Ripoti mpya ya maendeleo yam toto iliyozindiliwa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la kuhudumia Watoto duniani UNICEF inaelezea haja ya kutenga uwekezaji katika huduma ya lishe hususan katika nchi masikini na dhaifu zaidi huku miaka ya kwanza ya maisha ya mtoto ikitoa fursa zisizoweza kuelezeka za kuboresha afya ya maishani, lishe na ustawi.
  2. Tukisalia na masuala ya afya nusu ya watu wote duniani bado hawana huduma ya kutosha ya maji safi ya kunywa, usafi wa mazingira na kujisafi yaani WASH ambayo ingeweza kuzuia vifo vya watu milioni 1.4 na Maisha yaliyoboreshwa ya watu milioni 74 wenye ulemavu  hadi mwaka 2019 kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya kimataifa iliyotolewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na makala iliyochapishwa katika jarida la afya la Uingereza The Lancet.       
  3. Na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO pamoja na mashirika manne wadau, wamepewa jukumu la kuongoza mpango wa pamoja wa bahari safi na zenye afya, anmbao ni mradi unaolenga kuanzia kwenye chanzo taka hadi baharini  ambao utaelekeza ruzuku ya hadi dola milioni 115 kuzisaidia nchi kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ya pwani na mfumo mzima wa Maisha ya baharí.
  4. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma akitujuza walivyojiandaa kuadhimisha siku ya lugha ya Kiswahili duniani ambayo kilele chake ni Julai 7.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
15'37"