Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya: UNICEF
Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF unafanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine, lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.