Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 JUNI 2023

26 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia lugha ya Kiswhaili na ripoti ya dawa za Kulevya ya UNODC 2023. Makala tunakupeleka nchini Pakistan na mashinani nchini Kenya, kulikoni?

  1. Kuendelea kwa ongezeko la usambazaji haramu wa dawa za kulevya na mitandao ya usambazaji inayoendelea kukua inazidisha mizozo ya kimataifa na changamoto za huduma za afya na utekelezaji wa sheria, imesema Ripoti ya Dunia ya Dawa ya mwaka huu 2023 iliyozinduliwa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).
  2. Maadhimisho ya pili ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yatafanyika wiki ijayo Julai 7 na sasa maandali zi yanafanyika katika kila kona kuhakikisha siku hiyo iliyopewa uzito mkubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO lakini pia inatumika kama jukwaa la kuziunganisha jamii sio za Afrika tu zinazozungumza Kiswahili ali na nyinginezo zinazokumbatia Kiswahili.   
  3. Katika makala na leo ikiwa ni siku ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi Mabaya ya dawa Za Kulevya na Usafirishaji Haramu kauli mbiu ya mwaka huu inasema, “Watu kwanza: acha unyanyapaa na ubaguzi, imarisha kinga”. Tunaelekea nchini Pakistan kusikia kisa cha binti aliyedumbukia kwenye uraibu wa dawa za kulevya na kupoteza kila kitu.
  4. Mashinani tutaelekea Kalobeyei huko Kakuma nchini Kenya kusikiliza jinsi ambavyo wakimbizi wanavyoishi kwa utengamano na jamii za wenyeji nchini humo.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'26"