Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Dawa za kulevya

UNAMA / Eric Kanalstein

Mariam: Dawa za kulevya zilinifanya kupoteza mtoto na mume

Tatizo la dawa za kulevya duniani ni suala tata ambalo linaathiri mamilioni ya watu duniani kote. Watu wengi wanaotumia dawa za kulevya hukumbana na unyanyapaa na ubaguzi, jambo ambalo linaweza kudhuru zaidi afya yao ya kimwili na kiakili na kuwazuia kupata usaidizi wanaohitaji.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu UNODC inatambua umuhimu wa kuchukua mtazamo unaozingatia watu kuhusu sera za dawa za kulevya, kwa kuzingatia haki za binadamu, huruma na mazoea yanayotegemea ushahidi. 

Sauti
4'1"
UNODC

Usambazaji wa Dawa za Kulevya umezidisha mizozo ya kimataifa, ripoti ya UNODC yaonya

Kuendelea kwa ongezeko la usambazaji haramu wa dawa za kulevya na mitandao ya usambazaji inayoendelea kukua inazidisha mizozo ya kimataifa na changamoto za huduma za afya na utekelezaji wa sheria, imesema Ripoti ya Dunia ya Dawa za kulevya mwaka huu 2023 iliyozinduliwa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC). 

Sauti
3'23"
Mfanyakazi wa kikosi cha polisi wa kuzuia madawa ya kulevya nchini Liberia akiwa pembeni ya jalala la taka mjini Monrovia.
UN Photo/Staton Winter

Ripoti ya Dunia ya Dawa za Kulevya ya UNODC 2023 yaonya

Kuendelea kwa ongezeko la usambazaji haramu wa dawa za kulevya na mitandao ya usambazaji inayoendelea kukua inazidisha mizozo ya kimataifa na changamoto za huduma za afya na utekelezaji wa sheria, imesema Ripoti ya Dunia ya Dawa za kulevya mwaka huu 2023 iliyozinduliwa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).

Sauti
3'23"

26 JUNI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia lugha ya Kiswhaili na ripoti ya dawa za Kulevya ya UNODC 2023. Makala tunakupeleka nchini Pakistan na mashinani nchini Kenya, kulikoni?

Sauti
13'26"

09 MACHI 2023

Ni Alhamisi tulivu kabisa ya tarehe Tisa ya mwezi Machi mwaka 2023, siku ya mwisho ya mkutano wa 5 hapa Qatar wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani ambapo leo ni mada kwa kina na tutasalia hapa Doha, Qatar ambako katika mkutano waw a 5 wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani, LDC5, miongoni mwa washiriki ni vijana ambao walifika hapa kuhakikisha sauti zao zinakuwa sehemu ya maazimio ya mkutano huo. Miongoni mwa vijana hao ni Jadot Nkurunziza ambaye kwa kushirikiana na wenzake wanaunga mkono mkono mradi unaotekelezwa na Rais wa kurejesha misitu nchini Burundi kwa kupanda miti.

Audio Duration
12'5"