Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa ALiVE awamu ya pili kupima stadi za watoto nje ya masomo ya kawaida Zanzibar

Mradi wa ALiVE awamu ya pili kupima stadi za watoto nje ya masomo ya kawaida Zanzibar

Pakua

Baada ya kufanya tathmini ya upimaji Stadi za maisha na maadili kwa vijana wenye umri wa miaka 13  hadi 17 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, mradi wa ALiVE katika awamu ya pili umepanga kuwafikia watoto wenye umri wa miaka  6  hadi 12 ambao bado wako shule ili kuwapima viwango vyao vya Stadi za maisha na maadili ikiwa ni katika jitihada za kuchechemua fikra tunduizi na kusongeza malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs. 

Kama ambavyo mradi huu utatekelezwa katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki, Visiwani Zanzibar nako uzinduzi umefanyika na hapa Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM kutoka Morogoro, Tanzania amesafiri hadi Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani humo Zanzibar na kutuandalia na kutuandalia Makala hii. 

Audio Credit
Sarah Oleng'/Hamad Rashid
Audio Duration
5'34"
Photo Credit
Hamad Rashid