Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 JUNI 2023

21 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia Migogoro nchini Ukraine na wakimbizi nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Tanznai na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?  

  1. Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Matthew Hollingworth amelaani vikali shambulio lililofanywa na Urusi kwenye eneo la Kherson lililoathirika vibaya na mafuriko ya bwawa la Kakhovka, na kukatili maisha ya mfanyakazi wa ukoaji na kujeruhi wengine.
  2. Serikali ya Kenya inaendesha mradi wa “shiriki” ambao unawapa fursa wakimbizi wanaosihi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko katika kaunti ya Turkana nchini humo kujitegemea kwa kufanya kilimo cha mbogamboga kupitia chama cha ushirika wa wakulima. Serikali hiyo imetenga ekari 21katika kambi ya Kakuma ili kutumika katika mradi huo ambao sio tu unawapa lishe bora wakimbizi, matumaini na kipato lakini pia umekuwa neema kwa jamii za wenyeji. 
  3. Katika makala Mwandishi wa redio washirika wetu MVIWATA FM ya Tanzania anatupeleka visiwani Zanzibar ambako umezinduliwa mradi wa AliVE awamu ya pili unaolenga kupima stadi za maisha na maadili kwa wanafunzi Watoto wa umri wa miaka 6 hadi 12.
  4. Na mashinani leo ikiwa ni siku ya Yoda duniani      tunarejea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo alieleza kwa nini yoga ni muhimu katika maisha ya mwanadamu.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
13'20"