Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

siku ya bahari duniani

08 JUNI 2023

Hii leo ni siku mada kwa kina na jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya bahari inayohimiza kuhakikisha bahari inakuwa safi na yenye afya ili iweze kuihudumia vyema jamii tutaangalia namna taka zinazotolewa baharini zinavyoweza kutumika kama malighafi bora ndani ya jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo …. Na katika kujifunza kiswahili tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno"RUWI", salía hapo hapo!

Sauti
11'20"
Wavuvi pwani ya Kenya.
UN News/Thelma Mwadzaya

Tusipoilinda bahari tunaathiri kizazi cha sasa na vijavyo: Wananchi wa Vanga Kenya 

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani Umoja wa Mataifa imeichagiza dunia kuchukua hatua Madhubuti ili kuhakikishwa inalindwa kwa ajili ya maslhai ya kizazi cha sasa na kijacho kwani bahari sio tu inahakikisha uhakika wa chakula kwa mamilioni ya watu , bali pia ni moja wa muajiri mkubwa na inachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la dunia la kila mwaka.  

© Ocean Image Bank/Brook Peters

Tufundishe watoto wetu kulinda bahari 

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani, Umoja wa Mataifa unapazia sauti umuhimu wa kulinda  bahari ambayo ni chanzo cha zaidi ya asilimia 50 ya hewa ya Oksijeni inayotumika duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anaonya kuwa shughuli za binadamu zinachochea mambo makuu manne yanayotishia uhai wa bahari na viumbe vyake

Sauti
1'16"

08 Juni 2022

Jaridani Jumatano Juni 8-2022 na Leah Mushi

-Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani, Umoja wa Mataifa unapazia sauti umuhimu wa kulinda bahari ambayo ni chanzo cha zaidi ya asilimia 50 ya hewa ya Oksijeni inayotumika duniani.

-Shirika la Umoja wa Mataifa lakuhudumia watoto UNICEF limesema hali ni tete na watoto zaidi ya laki 3 na themanini wana utapiamlo mkali nchini Somalia ambapo hata ukiwaona watoto hao machozi yatakutoka.

Sauti
9'58"
UNDP/Azza Aishath

COVID-19 inatupa fursa na wajibu wa kuimarisha uhusiano wetu na asili: Guterres

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kumbusho kwamba binadamu wote wanahusiana wenyewe lakini pia na asili. Tupate ufafanuzi zaidi na Jason Nyakundi

Guterres ameyasema hayo kupitia ujumbe wake maalum wa siku hii ambayo kila mwaka huadhimishwa June 8 na kusistiza kwamba wakati dunia ikijitahidi kukomesha janga hili la COVID-19 na kujijenga upya ni fursa muhimu ya kubadilika

Sauti
1'56"

08 JUNI 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo Ikiwa ni siku ya bahari duniani 
-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la virusi vya Corona au COVID-19 ni kumbusho kwamba binadamu wote wanahusiana wenyewe lakini pia na asili.
-Nyongeza dola milioni 40 kusaidia DRC kukabili dharura ikiwemo Ebola
-FAO yasema Udhibiti wa uvuvi ni muhimu ni wakati wa kutumia kila kona
-Na kwenye Makala leo tutasikia kutoka kwa mwanamazingira kuangazia kwa undani vichocheo vya mafuriko ambayo tayari yamesababisha maelfu kwa maelfu kukosa makazi na kupoteza mali nc
Sauti
12'4"
Picha: Kwa hisani ya James Waikibia

Kumbe ndoto zangu kupinga matumizi ya plastiki sio za abunuwasi:Wakibia

James Waikibia kutoka county ya Nakuru nchini Kenya  amekuwa akibeba bango la kauli mbiu ya mwaka khuu ya kupinga matumizi ya plasiki kwa miaka sita sasa.

Na kampeini yake imekuwa ikijikita katika masuala mawili,  mosi  amekuwa akikusanya taka hizoza plastiki na kisha kuzichoma na pili kuandika makala mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii kuhusu taka hizo kwa lengo kuwachagiza wananchi kuachana na matumizi ya plastiki

Sauti
1'52"