Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 MEI 2023

15 MEI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tuanaangazi ripoti ya WHO ya vikoleza utamu visivyo sukari halisia, na huduma za afya zizazotolewa nchini Malawai kupitia kilniki za kuhama kwa njia ya magari.  Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, hii leo limetoa mwongozo unaoshauri watu wasitumie vikoleza utamu visivyo sukari halisia (NSS) kwa lengo la kupunguza uzito na kuepusha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs. 
  2. Wananchi wa Malawi walioathirika na Kimbunga Freddy wamepongeza mbinu ya kutumia kilniki za kuhama kwa njia ya magari iliyotumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwahudumia wanawake na watoto nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kilicholipiga eneo hilo takribani miezi mwili iliyopita.
  3. Katika Mkala, leo ikiwa ni siku ya familia duniani nakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mwandishi wetu George Musubao amemulika ni vipi familia inajitahidi kukidhi mahitaji licha ya changamoto za usalama.
  4. Katika mashinani na tutaelekea nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama linavyokuza nidhamu na kuboresha usafi shuleni.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha