Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 FEBRUARI 2023

28 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani mada kwa kina ambayo leo inatupeleka Kenya kuangazia umuhimu na faida za lugha mama. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ukame Pembe ua Afrika, wakimbizi nchini Somalia na watoto waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Uturuki . Mashinani tutakupeleka nchini Yemen, kulikoni?.

  1. Ukanda wa Pembe ya Afrika ukiingia msimu wa sita bila mvua, ukimbizi wa ndani unazidi kushamiri kwa kuwa mamilioni ya watu kutoka Somalia, Ethiopia na Kenya wanaendela kuhaha katikati ya uhaba wa maji, njaa, ukosefu wa usalama na mizozo, amesema Olga Sarrado, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Geneva, Uswisi.
  2. Tukisalia Pembe ya Afrika, hususan Somalia, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limesema idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Somalia ikifikia kiwango cha juu cha watu milioni 3.8, shirika hilo linategemea uwekezaji wa wahisani kwenye majawabu ya kuepusha zaidi ukimbizi wa ndani na kushughulikia mazingira duni ya maisha kwa mamilioni ya walioathiriwa na ukame na mzozo unaoendelea nchini humo.
  3. Na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Catherine Russell amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Uturuki na kusema watoto milioni 2.5 wanahitaji msaada wa dharura kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi  yaliyokuba kusini-mashariki mwa nchi hiyo na kaskazini mwa Syria mapema mwezi huu.
  4. Na katika mashinani tutaelekea Aden nchini Yemen ambako huko Bi. Fatima Muhammed Saeed mkimbizi wa ndani mwenye umri wa miaka 35 na mama wa watoto 9 anasema hapo awali kabla ya kukimbia vita maisha yalikuwa mazuri lakini sasa wanaishi maisha ya aibu na magumu mpaka hata kupata utapiamlo.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'55"