Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 FEBRUARI 2023

24 FEBRUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani linaangazia vita vya mwaka mmoja nchini Ukraine na kimbunga Freddy.  Makala na mashinani tunasalia huko huko Ukraine.

  1. Vita ya Ukraine ikiwa inaingia mwaka wake wa pili, wawakilishi mbalimbali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wametoa maoni yao kufuatia uamuzi kwa njia ya kura uliofanywa na Kikao Maalumu cha  dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio jipya la kutaka amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine na kwamba Urusi bila masharti yoyote iondoe mara moja majeshi yake katika ardhi ya Ukraine.
  2. Kimbunga Freddy moja ya vimbunga vilivyodumu kwa muda mrefu na kusababisha athari kubwa sehemu mbalimbali sasa kimeondoka Madagascar na kubisha hodi Msumbiji ambako kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kinaleta tishio kubwa kwa sababu ya kiwango cha mvua kinachoambatana nacho.
  3. Katika makala tunamulika mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
  4. Na katika mashinani mashinani tutasalia nchini Ukraine katika kituo cha muda cha watoto wakimbizi wa ndani nchini Ukraine kusikia ni jinsi gani wafanyakazi wa kujitolea wanavyowasaidia watoto hao kurejesha afya yao ya kiakili.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Duration
13'44"