Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 FEBRUARI 2023

23 FEBRUARI 2023

Pakua

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunabisha hodi kaunti ya Makueni Kenya kuangazia mchango na faida za mikunde kwa mazingira, wakulima na jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo afya ya uzazi, intaneti, na msaada wa kibinadamu mashariki ya katiKatika kujifunza Lugha ya Kiswahili tunakwenda Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA kuchambua neno MBWANDA.

  1. Kila baada ya dakika 2 mwanamke mwanamke mmoja anafariki dunia kutokana na ujauzito au wakati wa kujifungua duniani kote, imesema leo ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ikifichua vikwazo vya kutisha dhidi ya afya ya wanawake katika miaka ya karibuni wakati huu ambapo vifo vya wajawazito vimeongezeka au bado viwango vyake vimepungua katika takribani maeneo yote duniani.
  2. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa MAtaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay amefungua mkutano wa kimataifa kuhusu Intaneti kwa ajili ya Kuaminiana huko Paris, Ufaransa na kusema kuzidi kuyoyoma kwa mpaka kati ya ukweli na uongo na kukataliwa kwa taarifa za ukweli za kisayansi, hakukuanzia kwenye mitandao ya kijamii bali kukosekana kwa kanuni za udhibiti na usimamizi na ndio maana uongo unashamirishwa kuliko ukweli.
  3. Na nchini Syria, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limesafirisha kutoka Gazientep nchini Uturuki, shehena ya tani 34.5 ya vifaa vya matibabu kuingia kaskazini-magharibi mwa Syria kupitia vituo vya mpaka vya Bab Al-Hawa na Bab Al-Salama vikiwa na zaidi ya thamani ya dola milioni 353 ili kuimarisha huduma katika vituo vya afya ambavyo sasa vimezidiwa uwezo kufuatia tetemeko la ardhi lililokumba taifa hilo zaidi ya wiki mbili zilizopita.
  4. Na katika Lugha ya Kiswahili na leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA anafafanua neno MBWANDA.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'51"