Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 DESEMBA 2022

28 DESEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea habazi za UNCTAD na kazi za Umoja wa Mataifa nchini CAR. Makala tunakupeleka Karamoja nchini Uganda na mashinani tunakuletea ujumbe wa WFP kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

  1. Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD imesema mwaka huu wa 2022 umekuwa mgumu sana ambapo familia nyingi zimekuwa zikihaha kuweka mlo mezani na kujikimu hadi mwisho wa mwezi, lakini kuna suluhu na suluhu hizo zinapaswa kuwa za kimkakati na za kimataifa
  2. Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambapo alikutana na walinda amani na kufanya mikutano na viongozi wa kijeshi.
  3. Makala tunaelekea nchini Uganda katika eneo la Karamoja kuangazia namna shirika la Umoja la Afya Ulimwenguni linavyosaidiana na wadau wengine kutokomeza tatizo la utapiamlo mkali.
  4. Na mashinani leo tuko kwa mtaalam wa mabadiliko ya tabianchi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP Jacquline Tesha akifafanua ni kwa vipi janga la mabadiliko ya tabianchi linachochea zahma ya njaa duniani.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
9'58"