Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 DESEMBA 2022

19 DESEMBA 2022

Pakua
Hii leo jaridani tunakuletea habari kutoka mkutano wa COP 15, na nchini Tanzania, makala tunasalia nchini humo mkoani Morogoro na mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu bayoanuai. 1. Ikiwa leo ni tamati ya mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa kuhusu bayonuai, COP15, huko Montréal, Canada, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, limekaribisha makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa katika mkutano huo kuhusu mpango mpya wa kuhifadhi na kulinda asili kwa kutumia Mfumo mpya wa Kimataifa wa Bayonuai, (GBF). 2. Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani na masuala ya afya ya uzazi UNFPA nchini Tanzania limekabidhi jeshi la polisi mkoani Manyara msaada wa jengo la dawati la jinsia na watoto ikiwa njia moja wapo ya jitihada za kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia na mila kandamizi dhidi ya wanawake, wasichana na watoto. 3. Makala tunakwenda mkoani Morogoro, Mashariki mwa Tanzania ambako wadau wa maendeleo wamefanikisha ujenzi wa maktaba mtandao au Elibrary kwenye shule jumuishi. 4. Na mashinani tunamulika umuhimu wa kurithisha ufahamu kwa asili kwa vizazi ili kuhifadhi bayonuai. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Audio Duration
14'39"