Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 DESEMBA 2022

16 DESEMBA 2022

Pakua

Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 16  ya mwezi Desemba mwaka 2022 tunakuletea habari kuhusu uhamiaji na kazi za walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.  

  1. Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wahamiaji itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki Desemba 18 shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limemtaka kila mtu kutafakari je muhamiaji ni nani?
  2. Kikosi cha 5 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANZBATT 5 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, kimekamilisha muda wake  na kukipisha kikosi kingine cha 6 nacho kutoka Tanzania, TANZBATT 6 ambacho kitaendeleza jukumu hilo. Kutoka Berberat, Captain Mwijage Inyoma ni Afisa Habari wa TANZBATT 06 ametuandalia taarifa hii.  
  3. Katika makala tunakwenda nchini Kenya ambako sekta ya mahakama imejizatiti kuhakikisha kukatika kwa umeme hakuathiri utendaji kazi wao na kwa kushirikiana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu UNDOC wanatekeleza mradi uitwao PLEAD unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya EU ukilenga kuweka umeme unaotumia nishati ya jua katika mahakama na mahabusu.
  4. Na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC usikiliza ndoto ya mtoto mkimbizi ya kutaka  kuwa mwalimu.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, Karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'31"