Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 August 2020

04 August 2020

Pakua
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi
 -Janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kuripotiwa maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  amesema tuchukue maamuzi ya kijasiri kunusuru masomo wakati huu wa COVID-19.
-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limelaani vikali mauaji ya watu wapitao 18 katika kambi ya muda ya kuhifadhi wakimbizi wa ndani nchini Cameroon  

-Mkimbizi kutoka Syria anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jorda ameunda roboti kwa kutumia vifaa vya plastiki vya LEGO ambayo inasaidia kupambana na ugonjwa wa corona  

-Na leo kwenye Makala tutakwenda eneo la Maziwa, Kahawa West Nairobi Kenya kumsikia Lucy Wanjeri Njuguna ambaye amejiajiri kwa kuunda samani kutokana na tairi za magari zilizotumika. 

-Na kwenye  mashinani leo  tutakwenda nchini Rwanda kusikia jinsia wanafunzi wanavyotumia muda wao wakati huu ambapo shule zimefungwa Karibu!

 

 

 

 

 

 

 

 
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'4"