Chuja:

Anonio Guterres

04 August 2020

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Assumpta Massoi
 -Janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kuripotiwa maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  amesema tuchukue maamuzi ya kijasiri kunusuru masomo wakati huu wa COVID-19.
-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limelaani vikali mauaji ya watu wapitao 18 katika kambi ya muda ya kuhifadhi wakimbizi wa ndani nchini Cameroon  

-Mkimbizi kutoka Syria anayeishi katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari nchini Jorda ameunda roboti kwa

Sauti
11'4"
Katibu Mkuu António Guterres akizungumza kwenye kongamano la dunia la muungano  wa R20 nchini Austria
UNIS Vienna/Nikoleta Haffar

Komesheni ruzuku kwa sekta ya mafuta na matumizi ya fedha za watoa ushuru kutokomeza dunia- Guterres

Tunahitaji kutoza kodi uchafuzi wa hewa lakini sio watu na kukomesha ruzuku kwa sekta ya mafuta,  amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres hii leo Jumanne kwenye kongamano la dunia la muungano  wa R20, shirika  linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa lilioanzishwa na aliyekuwa gavana wa California nchini Marekani Arnold Schwarzenegger.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akitoa ripoti yake ya kila mwaka kabla ya kuanza kwa mkutano wa baraza kuu wa 73
UN Photo/Cia Pak

Si hiyari, ni lazima kulikabili jinamizi la mabadiliko ya tabia nchi:Guterres

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 73 umefunguliwa rasmi hii leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Wawakilishi kutoka nchi 193 wanachama, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo wakikutana kwa lengo la kuhakikisha ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa inatimia ifikapo 2030.