Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 Agosti 2019

20 Agosti 2019

Pakua

Je wafahamu kuwa mwanamke mmoja raia wa Cameroon alilazimika kuwavisha wanae wa kiume hijab na sketi ili wasichukuliwe na magaidi wa Boko Haram? Pata basi kisa hiki kwenye jarida letu la leo sambamba na taarifa kutoka Libya kuhusu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwenye mji wa kusini wa Murzuq. Nchini Msumbiji nako madhila ya vimbunga yaendelea kusalia miongoni mwa wananchi, mkuu wa IOM afanya ziara na makala leo ni wanawake ambapo Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Rachel Shebesh, Katibu Tawala kwenye Wizara ya masuala ya jinsia, wazee na watoto nchini Kenya  huku mashinani tukimsikia Mzee Ali Haji ambaye ni Naibu  Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, anazungumzia maswala ya kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za bahari katika  mkataba wa kimataifa wa matumizi ya baharí UNCLOS.

Audio Credit
Grace Kaneiya
Audio Duration
11'49"