Ukatili uliofanywa na waasi wa ISIL Iraq ni wa kutisha na unaweza kuwa ni uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu, imesema leo ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa. Pia imeelezea kugundulika kwa makaburi ya halaiki zaidi ya 200 huku manusura wakielezea madhila waliyopitia mikononi mwa kundi hilo la ISIL