12 Septemba 2018

12 Septemba 2018

Hii leo jaridani Anold Kayanda anaanzia kwenye makao makuu  ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambako Baraza la Usalama limejadili jinsi ya kuimarisha  ulinzi wa amani hususan usaizidi kwa nchi zinazochangia walinda amani. Ni kwa muktadha huo mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ amezungumza na Idhaa hii kuona kile ambacho Tanzania inataka kuona kinafanyika. Kayanda anamulika pia jukwaa la kimataifa la kuchagiza biashara ya nje lililomalizika leo huko Zambia na kijana mmoja kaelezea imekuwaje amefanikiwa katiak biashara yake ya njugu na maembe ya kukausha. Makala ni kijana wa kike aliyetaka kujiua kulikoni? Na mashinani tunakwenda Kenya, riwaya na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili. KARIBU

Audio Credit:
Anold Kayanga
Audio Duration:
12'18"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud