Chuja:

ITC

25 Mei 2021

Hii leo jaridani tunaanzia huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika janga la mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini.  Kisha tunaangazia ripoti ya UNICEF ya kwamba ukosefu wa maji ni silaha hatari zaidi kuliko hata mabomu kwa watoto. Nchini Tanzania kijana Aisha Kingu atumia mashairi kuelimisha watu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Makala tunarejea DRC kuangazia ziara ya Mkuu wa UNFPA katika hospitali ya Panzi jimboni Kivu Kusini na tunakunja jamvi na mashinani huko Uvinza kwa wachimba madini ya chumvi.

Sauti
13'36"
UN News/Matt Wells

Mitaji mikubwa kwenye biashara ndogo na za kati kufanikisha SDGs- ITC

Kuelekea siku ya biashara ndogo na za kati, SMEs hapo kesho, Umoja wa Mataifa umetaka uwekezaji zaidi kwenye biashara hizo kwa kuwa ndio msingi wa kufanikisha maleng ya maendeleo endelevu, SDGs. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Kituo cha biashara cha kimataifa, ITC ambayo ni ofisi tanzu ya kamati  ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, imesema hayo kupitia ripoti yake mpya iliyotolewa wiki hii ikisema kuwa msisitizo ni biashara ndogo na za kati kwa kuzingatia mambo makuu manne.

Sauti
2'7"

12 Septemba 2018

Hii leo jaridani Anold Kayanda anaanzia kwenye makao makuu  ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambako Baraza la Usalama limejadili jinsi ya kuimarisha  ulinzi wa amani hususan usaizidi kwa nchi zinazochangia walinda amani. Ni kwa muktadha huo mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ amezungumza na Idhaa hii kuona kile ambacho Tanzania inataka kuona kinafanyika.

Sauti
12'18"
UN Photo/Martine Perret

Toka chupa za taka hadi mapambo ya ndani

Jukwaa la kimataifa la uendelezaji wa biashara ya nje, WEDF limeanza leo huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia likileta pamoja viongozi wa serikali na wafanyabiashara kwa lengo la kufungua milango ya biashara ya nje duniani.

Miongoni mwa washiriki ni Beatrice Nyatando, kutoka Zambia, mbunifu mitindo mbobezi ambaye amegeukia biashara ya kuokota chupa zilizotupwa ziwe za plastiki au za kupasuka na kuzigeuza mapambo.

Akihojiwa na Stella Vuzo wa Umoja wa Mataifa kando mwa jukwaa hilo, Bi. Nyantando ambaye sasa anauza chupa moja kwa dola tano amesema..

Sauti
1'20"