Skip to main content

Chuja:

WEDF2018

13 Septemba 2018

Mwendazake Kofi Annan, azikwa leo huko Ghana, Katibu Mkuu Antonio Guterres afunguka. Keating ahitimisha jukumu lake Somalia apazia sauti vyombo vya kimataifa vya  habari. Kutoka Zambia baada ya jukwaa, wajasiriamali sasa kuhaha na serikali zao ili kukuza biashara ya nje. Na makala leo tunabisha hodi Uganda kunani? Na mashinani ni maoni yako kutoka Facebook kuhusu Kofi Annan. Karibu na mwenyeji wako leo ni Anold Kayanda

Sauti
11'14"

12 Septemba 2018

Hii leo jaridani Anold Kayanda anaanzia kwenye makao makuu  ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambako Baraza la Usalama limejadili jinsi ya kuimarisha  ulinzi wa amani hususan usaizidi kwa nchi zinazochangia walinda amani. Ni kwa muktadha huo mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ amezungumza na Idhaa hii kuona kile ambacho Tanzania inataka kuona kinafanyika.

Sauti
12'18"
UN Photo/Martine Perret

Toka chupa za taka hadi mapambo ya ndani

Jukwaa la kimataifa la uendelezaji wa biashara ya nje, WEDF limeanza leo huko Lusaka, mji mkuu wa Zambia likileta pamoja viongozi wa serikali na wafanyabiashara kwa lengo la kufungua milango ya biashara ya nje duniani.

Miongoni mwa washiriki ni Beatrice Nyatando, kutoka Zambia, mbunifu mitindo mbobezi ambaye amegeukia biashara ya kuokota chupa zilizotupwa ziwe za plastiki au za kupasuka na kuzigeuza mapambo.

Akihojiwa na Stella Vuzo wa Umoja wa Mataifa kando mwa jukwaa hilo, Bi. Nyantando ambaye sasa anauza chupa moja kwa dola tano amesema..

Sauti
1'20"