Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka Nairobi hadi Kigali- Uhamiaji halali wazaa matunda

Kutoka Nairobi hadi Kigali- Uhamiaji halali wazaa matunda

Pakua

Uhamiaji barani Afrika unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi endelevu na kuleta mabadiliko stahili ya kiuchumi kwa nchi husika iwapo kutakuwepo na mifumo bora ya kisera kuhusu uhamiaji.

 

Kamati ya maendeleo ya biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema hayo leo kwenye ripoti yake ya maendeleo barani Afrika,  ikiangazia zaidi marekebisho ya mfumo wa uhamiaji ili uwe na manufaa.

 

Ripoti hiyo pamoja na kuonyesha kuwa waafrika siyo tu wanakimbilia Ulaya bali pia wanahamia nchi nyingine za Afrika, imetaja mafanikio ya uhamiaji wa ndani Afrika uliochochewa na mifumo bora iliyowekwa na nchi za Afrika.

 

Mifano hiyo ni mingi lakini Jane Muthumbi, afisa wa UNCTAD, huko Geneva, Uswisi amezungumza na Idhaa hii na kutaja baadhi.

 

(Sauti ya Jane Muthumbi)

 

Ripoti hii inayoonyesha kuwa Afrika sasa nalo ni eneo ambako wahamiaji kutoka bara hilo wanahamia, ina lengo la kusaidia kuimarisha msimamo wa Afrika katika makubaliano ya kimataifa ya uhamiaji yanayotarajiwa kupitishwa mwezi disemba mwaka huu huko Marrakesh, Morocco.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'58"
Photo Credit
Watu wakitumia intaneti jijini Nairobi, Kenya.(Picha: ITU/G. Anderson)