Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama umasikini ungekuwa na sura, basi ni ya mwanamke wa kijijini: IFAD

Kama umasikini ungekuwa na sura, basi ni ya mwanamke wa kijijini: IFAD

Pakua

Hayo yamesemwa na makamu wa Rais wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD, Bi Cornelia Richter akizungumza na UN news kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW62, unaoendelea Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New york Marekani.

(SAUTI YA CORNELIA RICHTER)

‘Endapo umasikini ungekuwa n asura basi ingekuwa ya mwanamke wa kijijini, sisi hapa IFAD tunajaribu kuwekeza katika uwezo wa wanawake na sio kuwadhalilisha wanawake”

Amesisitiza kuwa kuboresha maisha yao ni muhimu ili kutokomeza umasikini, jambo ambalo litahitaji mtazamo tofauti na hatua mbalimbali kulifanikisha ikiwemo

(CORNELIA RICHTER )

“Mosi ni kuhakikisha kwamba vikwazo vya kisheria vinaondolewa katika baadhi ya masuala, pia kuhakikisha kwamba mtazambo wa  jinsia unajumuishwa katika sera za kilimo, pia kuhakikisha kwamba tunaimarisha taasisi za vijijini na kuwekeza katika uwezeshaji wa maendeleo kwa ajili ya wanawake na wasichana wa vijijini, ili kuhakikisha kwamba wanatambua kikamilifu uwezo wao.”

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'23"
Photo Credit
Mwanamke mkulima akiwa shambani nchini Nepal:Picha na UN Women