Chuja:

vijijini

20 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora ucha kutoka Umoja wa Mataifa anakuletea

- Serikali ya Tanzania yaitikia wito wa shirika la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO na leo imezindua mkakati wa ufundishaji kupitia teknolojia ya Radio na Televisheni kuhakikisha watoto wanasoma wakati huu wa COVID-19

- Mabalozi wema wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD Idris Elba na mkewe sabrina Elba leo wamezindua mfuko na ombi la dola milioni 200 kuwasaidia wakulima vijijini wakati huu wa janga la Corona ili kuhakikisha uhakika wa chakula

Sauti
13'24"

Kama umasikini ungekuwa na sura, basi ni ya mwanamke wa kijijini: IFAD

Hayo yamesemwa na makamu wa Rais wa mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD, Bi Cornelia Richter akizungumza na UN news kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW62, unaoendelea Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New york Marekani.

(SAUTI YA CORNELIA RICHTER)

‘Endapo umasikini ungekuwa n asura basi ingekuwa ya mwanamke wa kijijini, sisi hapa IFAD tunajaribu kuwekeza katika uwezo wa wanawake na sio kuwadhalilisha wanawake”

Sauti
1'23"