Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gari za wagonjwa zahitajika kuokoa majeruhi magharibi mwa Mosul-WHO

Gari za wagonjwa zahitajika kuokoa majeruhi magharibi mwa Mosul-WHO

Pakua

Vita vinavyoendelea baina ya vikosi vya serikali ya Iraq na magaidi wa ISIL vimelifanya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutuma magari zaidi ya kubeba wagonjwa ili kusaidia kutibu majeruhi wanaokimbia vita hivyo magharibi mwa Mosul.

Vita hivyo vilivyoanza tangu mwanzo wa Oktoba mwaka jana, vimejeruhi zaidi ya watu 1,900 ambao wametibiwa katika hospitali ya Ninewa na maeneo ya karibu.

Serikali na vikosi vya muungano vinaendelea na mashambulizi mitaa hadi mitaa iliyo na misindiko ya watu katika harakati za kukomboa magharibi mwa Mosul ambayo bado imeshikiliwa na magaidi wa ISIL.

WHO ikishirikiana na Shirika la Chakula Duniani WFP wamepelekamagari ya wagonjwa 15 na vifaa vya matibabu, ili kuboresha na kupunguza muda wa kusafiri na kutoa tiba.

Photo Credit
Magari ya wagonjwa huko Iraq.(Picha:WHO)