Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simu ndio daraja kati ya waliosalia Syria na wakimbizi kwingineko

Simu ndio daraja kati ya waliosalia Syria na wakimbizi kwingineko

Pakua

Wakati mzozo wa Syria unaendelea kushuhudiwa ukiingia mwaka wa saba, raia wanakimbilia nchi jirani kuomba hifadhi. Mara nyingi wakimbizi hao kutoka Syria wanajikuta kwenye kambi zenye mazingira ya upweke huku baadhi yao mawazo yakisalia kwa familia zilizobakia nchini Syria.

Katika makala hii na Flora Nducha tunakutana na kijana Abdalla ambaye yuko na babake kambini Za’atari nchini Jordan na anasema simu ni teknolojia muhimu kwani ni daraja kati ya familia walioko Syria na wale waliokimbilia kwingineko. Basi ungana na Flora Nducha kupata undani wa Makala hii.

Photo Credit
Mtoto Abdalla na babake wakitafuta mtandao wa kupiga simu. (Picha:UNHCR/video capture)