Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zahma ya watu kufurushwa makazi yao Mosul inaendelea-UNHCR

Zahma ya watu kufurushwa makazi yao Mosul inaendelea-UNHCR

Pakua

Hivi sasa kuna Wairaq zaidi ya laki tatu ambao ni wakimbizi wa ndani kutoka Mosul na viunga vyake tangu kuanza kwa operesheni za kijeshi za kuukomboa mji huo 17 Oktoba 2016.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR msaada umeshasambazwa kwa wakimbizi wa ndani 234,000 kwenye kambi zilizojengwa na shirika hilo.

Wakimbizi wengine zaidi ya 250,000 wanahifadhiwa katika nchi jirani ikiwemo Syria. UNHCR inasema ombi la dola milioni 578 limetolewa kwa ajili ya wakimbizi wa ndani na wakimbizi wengine katika kanda, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa mshikamano na watu wa Mosul waliosambaratishwa na vita.

Kwa hivi sasa UNHCR imetoa ombi lingine la dola milioni 212 kwa ajili ya kuendelea kutoa msaada muhimu kwa wakimbizi wa ndani mwaka 2017 zikiwemo dola milioni 37 zinazohitajika haraka.

Photo Credit
Watoto wakimbizi wa ndani Iraq wanburuta magodoro na vifaa vingine kuelekea makazi yao katika kambi ya Hasansham, Iraq.Picha: © UNHCR/Ivor Prickett