Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wapongeza Marekani kuondoa sheria baguzi

Wataalamu wa UM wapongeza Marekani kuondoa sheria baguzi

Pakua

Kubaguliwa kwa misingi ya rangi au kidini hadi sasa hakujaleta ufanisi wowote kwenye vita dhidi ya ugaidi, wamesema wataalam wawili wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

Ahmed Shaheed na Mutuma Ruteere wamesema hayo wakiangazia Marekani ambayo imefuta sheria iliyoanzishwa baada ya shambulizi la mwezi Septemba mwaka 2011 linaloweka vigezo vikali vya kuingia na kutoka nchini humo kwa raia kutoka nchi 25 za Mashariki ya Kati, Asia ya Kusini au Afrika ya Kaskazini, uitwayo NSEERS.

Wataalam hao wamesema mikakati fanisi ya kukabiliana na ugaidi na sheria haipaswi kuzingatia mawazo potofu au kutoelewa kwa makundi ambayo wengi wao wanahusika na msimamo mkali au vikundi vyenye msimamo mkali.

Wamesema mikakati ya udhibiti inafaa iandaliwe kwa kuzingatia ushahidi ili kuhakikisha ufahamu sahihi wa masuala ya kitaifa na mitaa na sio jamii au vikundi vya kikabila au kidini kunyanyapaliwa au kubaguliwa.

Photo Credit
Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu. Picha: Umoja wa Mataifa/ Jean-Marc Ferré