Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulimwengu unakabiliwa na ongezeko la tishio la silaha za nyuklia: IAEA

Ulimwengu unakabiliwa na ongezeko la tishio la silaha za nyuklia: IAEA

Pakua

Leo ni siku ya kutokomeza silaha za nyuklia duniani ambapo pia kumefanyika kikao cha 60 kuhusu nishati ya nyuklia jijini New York, Marekani.

Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA Dkt. Yukiya Amano amesema bado kuna changamoto katika udhibiti wa nyuklia.

Ametaja changamoto kuwa ni pamoja na ufuatiliaji wa silaha za nyuklia Iran, lakini kubwa zaidi ni majaribio ya silaha za nyuklia yanayofanywa mara kwa mara katika Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK, amenukuliwa akisema...

Mpango wa nyuklia wa DPRK- ambayo imefanya majaribio mawili ya nyuklia mwaka huu- bado ni suala lenye kuleta wasiwasi mkubwa. Ni tishio la amani na usalama katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Asia na kwingineko. IAEA iko tayari kuanza kazi zake za uchunguzi DPRK mara baada hali ya kisiasa itakaporuhusu".

Kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema kuna ongezeko la maombi ya msaada kutoka nchi wanachama katika kufanikisha malengo hayo hususan katika masuala ya nishati.

Hata hivyo amesema kazi ya shirika lake katika nyanja hii haipewi kipaumbele kinachostahili akigusia suala la upungufu wa fedha.

Photo Credit
UN Photo/Rick Bajornas)