Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi wa kibinadamu wahitajika Iraq

Msaada zaidi wa kibinadamu wahitajika Iraq

Pakua

Katika uzinduzi wa pamoja mjini Baghdad leo serikali ya Iraq na Umoja wa Mataifa wametoa witio kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kukabiliana matatizo ya mahitaji ya kibinadamu yanayoengezeka kwa kasi nchini Iraq.

Wairaq milioni 10 karibu theluthi moja wa idadi ya watu wote nchini humo wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu , ikiwa ni pamoja na watu milioni 3.3 ambao wamezikimbia nyumba zao tangu mwaka 2014.

Maelfu ya raia wa Iraq wako katika maeneo yaliyozingirwa  na majeshi yanayopigana , hawawezi kutoroka au kusaka usalama, kwa kuongezea watu wakimbizi wa Syria 250,000 wametafuta hifadhi nchini Iraq na wengi wao kwenye jimbo la Kurdistan ambako zaidi ya watu milioni moja wakimbizi wa ndani wanaishi, na baadhi yao wamerejea makwako wakijaribu kujenga upya maisha yao.

Photo Credit
Hapa ni Zahko nchini Iraq wanaume wabeba vifaa vya kukabiliana na baridi.(Picha:OCHA/Iason Athanasiadis)