Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na Bank ya dunia kuzindua jopo maalumu kwa ajili ya maji

UM na Bank ya dunia kuzindua jopo maalumu kwa ajili ya maji

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Bank ya dunia, Jim Yong Kim kwa pamoja wametangaza nia ya kuunda jopo jipya la kuchagiza hatua za haraka kuelekea lengo la maendeleo endelevu la maji na usafi (SDG 6) na mengine yanayoshabihiana.

Lengo la maendeleo endelevu nambari 6 linahakikisha uwepo na uendelevu wa maji na usafi kwa wote.

Tangazo hilo limekuja wakati ambapo nchi zinashuhudia shinikizo na majanga yanayoambatana na maji ambayo yatazidi kuwa mabaya kutokana na mabadiliko ya tabia nchi endapo hakutakuwa na maamuzi bora ya sera.

Ameongeza kuwa jopo hilo litasaidia kuchagiza hatua zinazotakiwa ili kugeuza mawazo kuwa ukweli. Mfumo wa Umoja wa mataifa ikiwemo UN water na mfumo wa maendeleo wa UM vimejidhatiti kupigia chepuo hatua jumuishi zinazoongozwa na nchi kuhusu utekelezaji wa SDG 6 na malengo mengine.

Jopo hilo litakaloongozwa na Rais wa Mauritius na Mexico litajumuisha wakuu wa nchi zilizoendelea na zinazoendelea likiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Rais wa Bank ya dunia katia kuchagiza hatua na kuongeza uwekezaji wa maji.

Photo Credit
Mtoto akisubiri wakati mama yake akijaza kipipa cha maji. Picha ya UN/Tobin Jones