Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya mama na mustakhbali wake

Lugha ya mama na mustakhbali wake

Pakua

Tarehe 21 mwezi Februari kila mwaka ni siku ya lugha ya mama duniani! Lengo ni kuhamasisha matumizi ya lugha ya mama katika  nyanja mbali mbali ikiwemo kielimu. Kila msichana na mvulana, mwanamke na mwanamume ni lazima awe na nyenzo muhimu kama vile lugha ili aweze kushiriki katika maswala muhimu katika jamii popote alipo.Licha ya umuhimu wa lugha ya mama, baadhi ziko hatarini kutoweka.Kauli mbiu mwaka huu ni  elimu jumuishi kupitia lugha; Lugha ina umuhimu! ambapo katika ujumbe wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova amesema kwamba ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 ni lazima iweke kipaumbele kuendeleza elimu sahihi kwa wote kwa kupanua upatikanaji wa elimu, kuzingatia usawa na ujumuishwaji na kuendeleza elimu kwa watu wote kote ulimwenguni kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kenya nchi iliyoko Afrika Mashariki ina jamii tofauti zenye lugha za mama mbali mbali .Lakini kuna lugha ambazo huenda zikatoweka kwani jamii hizo zinalandana na zingine kwa kutumia lugha na tamaduni za wengine. Basi ungana na Geoffrey Onditi wa radio washirika KBC ambaye alikutana na wanaharakati wawili wanaoendeleza lugha ya Kiburji, moja ya lugha ambazo ziko hatarini kutoweka hapa anazungumza na Paul Hirbo kutoka shirika la African Minority Empowerment Support Programme

Photo Credit
@UNESCO