Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sijakata tamaa licha ya hali tete Darfur: Luteni Jenerali Mella

Sijakata tamaa licha ya hali tete Darfur: Luteni Jenerali Mella

Pakua

Lazima kuileta amani kwanza ndiyo  tuilinde. Ni kauli ya mkuu wa vikosi vya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika jimboni Darfur nchini Sudan  UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella katika mahojiano na idhaa hii baada ya kuhitimishwa kwa mkutano uliowaleta pamoja wakuu wa vikosi vya kulinda amani mjini New York.

Luteni Jenerali Mella ambaye amefanya mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii anasema licha ya hali ya sintofahamu inayoendelea jimboni humo ambapo watu kadhaa wamepoteza makazi kutokana na mapigano ya kikabila, bado hajakata tamaa na anaelekeza nguvu zake kuhakikisha vikundi ambavyo havijasaini makubalino ya amani vinafanya hivyo.

Kwanza mkuu huyo wa vikosi vya UNAMID anaanza kwa kueleza wajibu na ukubwa wa kikosi anachokiongoza.

Photo Credit
Mkuu wa UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella.(Picha ya UM/idhaa ya kiswahili/Joseph Msami)